HISTORIA YA
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA BARA
Huduma ya zimamoto Tanzania Bara zilianza wakati wa utawala
wa Kikoloni mara tu baada ya vita vya pili vya Dunia mwaka 1945, na kwa kipindi hicho kulikuwa nakikosi kimoja kilichojulikana
kwa jina la POLICE
FIRE BRIGADE kilichosimamiwa na jeshi la Polisi.
Mnamo mwaka 1950
kikosi hiki kiligawanywa katika makundi mawili Zimamoto chini ya Halimashauri
za Manispaa na usimamizi wake ukawa chini ya Manispaa na kundi la pili ilikuwa
Zimamoto chini ya viwanja vya Ndege
chini ya usimamizi ya Idara ya Kazi kwa maana hiyo ilihama kutoka katika
usimamizi wa Jeshi la Polisi.
Kwa kuwa miji ilikuwa inakuwa kwa kasi hivyo basi vikosi
vingine vikaanzishwa na kimoja wapo ni kikosi cha Zimamoto bandari ambacho
kilikuwa chini ya usimamizi wa bandari.Mnanmo mwaka 1982 Zimamoto chini ya viwanja vya ndege ilihama na kuwa chini ya
usimamizi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi,wakati huohuo vikosi vya zimamoto
vilivyo kuwa chini ya Manispaa na miji viliwekwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za mikoa na serikari za mitaa(TAMISEMI)
Lengo la zimamoto kuanzishwa ilikuwa ni kutoa huduma ya
uzimaji wa moto pindi moto unapotokea na kufanya maokozi kwa ufanisi
zaidi,lakini kutokana na kuwa katika usimamizi wa mamlaka tofauti ufanisi wa
utendaji kazi wake haukuwaridhisha
viongozi wa serikali na ndipo serikali ikaamua kufanya mikakati ya kuboresha
huduma hiyo.
Katika bunge la Jamuhuri la Muungano wa Tanzania la mwaka 1985 sheria namba tatu(3) ilianzishwa
na kusababisa uanzishwaji wa Jeshi la Zaimamoto n Uokoaji lengo likiwa utowaji
wa huduma hiyo ya zimamoto itolewe katika taratibu na nidhamu ya kijeshi na kwa
kipindi hicho iliwekwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwakuwa lengo la uboreshaji wa huduma za zimamoto na uokoaji
zilikuwa bado zinahitajika,mnamo mwaka 2007
kwa mara nyingine tena Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha
sheria Na.14 ya Zimamoto na Uokoaji (Fire And Rescue Force Act) na baada ya hii
sheria jeshi la zimamoto na uokoaji liliwekwa chini ya Kamandi moja tofauti na
hapo awali.Kwa sheria hii Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilibadirisha muundo wa
Jeshi na kuweka mgawanyo mwa majukumu ilikuleta tija ili kurahisisha suala zima
la utowaji wa huduma za zimamoto na uokoaji.
Hivyo kwa sasa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaongozwa na
Kamishna Jenerali akisaidiwa na Naibu Kamishna Jenerali akifuatiwa na Kamishna
watatu wa divisheni tatu wanazoziongoza ambazo ni Utawala na Fedha,oparesheni
na Usalama wa umma na mali zao.
Katika divisheni hizi tatu kuna makamishna
wasaidizi wanaoziongoza ilikutengeneza mfumo wa utendaji wenye kuleta Tija na
katika utoaji wa huduma kwa jamii.
Kwa upande wa Usalama wa Umma idara
hii huusika na Kuzuia na kukabiliana na majanga ya aina yote kama
,Moto,matetemeko, Mafuliko na majanga mengine yanapotokea pia kufanya uchunguzi
wa vyanzo vya majanga yaliyokwisha tokea ili kupanga mikakati ya njisi ya
kukabiliana nayo.Pia huusika na utoaji wa elimu kwa umma juu ya majanga ya
moto,ukaguzi wa kinga na tahadhari ya majanga ya moto,Kukagua usalama wa ujenzi
katika viwanda vituo vya mafuta,kemikali na vituo vinavyo zalisha gesi na
kuhifadhi gesi.
Kwa upande wa Oparesheni miongoni
mwa majukumu yake ni pamoja na kusimamia mafunzo,kukagua huduma za zimamoto na
uokoaji kwa kanda na kufanya tathimini ya madhara yaliyotokea kwenye majanga
mbalimbali
Upande wa Utawala rasilimali watu na
Fedha majukumu yake ni kufanya utafiti na mafunzo,kusimamia uajili,kuandaa na
kutunza kumbukumbu za watumishi pamoja na maandalizi ya mpito ya sheria ya Moto
na uokoaji na kanuni zake.
Mbali na kuwa na changamotonyingi
lakini jeshi hili limekuwa na mafanikio makubwa moja wapo ikiwa ni kuanzishwa
kwa vituo vingi vya zimamoto takribani katika kila Mkoa na baadhi ya Wilaya
nchini,pia fanikio jingine ni suala zima la ushirikiano wa Jeshi la Zimamoto na
uokaji na majeshi Mengine kama vile
Magereza kwa kukubali mafunzo ya uaskari
kufanyika katika vyuo vyao kwa ngazi ya awali,uongozi mdogo,wakati na wajuu
kabisa.
Polisi kwa kukubali kutumia siraha
zao pindi zinapokuwa zinahitajika kwa mfano katika shughuli mbalimbali za jeshi
la zimamoto na ushirikiano mwingine wa majukumu ya kiulinzi katika nchi yetu
kwa ujumla.
Jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) kukubali baadhi ya askari wa
zimamoto kupatamafunzo katika chuo chao cha AirWing,Kimbiji vilivyopo Dar es
salaam,pamoja na kushirikiana katika majanga mbalimbali yenye kutishia maisha
ya watu na mali zao mfano,Mafuliko,Mlipuko wa mabomu ajari mbalimbali nk.
Pia kwa sasa Jeshi la zimamoto na
uokoaji Tanzania lina chuo chake binafsi kinachotoa mafunzo ya uaskari kwa
ngazi zote kuanzia mafunzo ya awali,vyeo vya kati na vya juu kilichopo wilaya
ya Handeni mokoaniTanga katika eneo liitwalo Chogo.
Tisocera steel - Titanium Hockey Club - The
JibuFutaTisocera ford escape titanium for sale steel. Stainless titanium 3d printing Steel. Steel. titanium plate flat irons $0.99. Steel. $17.00. Tisocera steel. Stainless titanium ring Steel. Stainless Steel. Stainless Steel. Stainless titanium blade Steel.