JESHI LA ZIMAMOTO MBEYA NAMBA YA DHARURA DHIDI YA MAJANGA YA MOTO RESCUE MATUKIO YOYOTE PIGA NAMBA YA DHARURA NI 114 ONYO SIO NAMBA YA KUCHEZEA ATAKAYE BAINIKA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YA MHUSIKA
Jumapili, 18 Septemba 2016
FIRE AND RESCUE FORCE MBEYA: Timu ya jeshi zimamoto mkoa wa mbeya yashiriki mic...
FIRE AND RESCUE FORCE MBEYA: Timu ya jeshi zimamoto mkoa wa mbeya yashiriki mic...: Timu ya jeshi zimamoto mkoa wa mbeya yashiriki michezo mbalimbali zidii ya timu ya jeshi la wananchi 44kj mbalizi.mchezo uliodhuruwa na waku...
Timu ya jeshi zimamoto mkoa wa mbeya yashiriki michezo mbalimbali zidii ya timu ya jeshi la wananchi 44kj mbalizi.mchezo uliodhuruwa na wakuu wa vikosi vyote vya jeshi la zimamoto FRF na jwtz.ikiwa ni jitihada za kuimarisha umoja wa vyombo vya ulinzi wa mkoa wa mbeya
kikosi cha zimamoto mkoa wa mbeya kikiwa tayari kwa mpambano kikiongozwa na assintant insepector Nyarusi na msaidizii wake assintant inspector Pati.
Timu ya zimamoto mkoa wa mbeya ikiwa inapasha misuli ilikukabiliana na timu ngumu ya 44jwtz katika bonanza la michezo ambapo timu ya 44jwtz iliibuka mshindi[44jwt 2-[0]FrF
kikosi cha zimamoto mkoa wa mbeya kikiwa tayari kwa mpambano kikiongozwa na assintant insepector Nyarusi na msaidizii wake assintant inspector Pati.
Timu ya zimamoto mkoa wa mbeya ikiwa inapasha misuli ilikukabiliana na timu ngumu ya 44jwtz katika bonanza la michezo ambapo timu ya 44jwtz iliibuka mshindi[44jwt 2-[0]FrF
mwamuzii wa mchezo akitoa maelezo kabla ya mchezo
golikipa wa timu ya zimamoto mkoa wa mbeya FC Rahim adamson(maarufu NGINGI ).akiwa tayari kwa mchezo huo mkali.
Imeletwa kwenu na kitengo cha habari 'JESHI LA ZIMAMOTO MBEYA
KWA MATUKIO MBALIMBALI YA MOTO MAJANGA YA AJALI
PIGA SIMU No 114.(Fc oscar watson mswima )
I
Ijumaa, 9 Septemba 2016
Alhamisi, 8 Septemba 2016
UCHANGIAJI WA DAMU KUOKOA MAISHA
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania inaungana na watu wengine kushiriki katika kampeni ya uchangiaji Damu wa hiari kwani Uchangiaji wa Damu ni Zawadi ya maisha.
NANI ANASTAHILI KUCHANGIA DAMU:-
Kuchangia Damu ni Kuokoa maisha ya Mtu mmoja au zaidi,na hii ni Zawadi kubwa ambayo binadamu anaweza kuumpa binadamu mwenzie.
Imeelezwa kuwa kuchangia Damu mwanamke anaweza kuchangia mara tatu(03) kwa Mwaka na mwanaume anaweza kuchangia mara nne(04) kwa Mwaka.
Kwa kawaida mwili wa mwanadamu una damu galoni tano(05) hadi saba(07), na kwa kawaida unapochangia Damu kiasi cha Mililita 450 kinachotolewa.Mchangiaji hubaki na kiasi cha kutosha cha Damu hakuna haja ya kuwa na hofu.
MUHIMU:
Mtu yeyote mwenya magonjwa ya kurith haruhusiwi kuchangia damu.
NANI ANASTAHILI KUCHANGIA DAMU:-
- Mtu yeyote mwenye umri kati ya 18 hadi 65.
- Mwenye uzito usiopungua kilo 65
- Awe na Afya Njema.
Kuchangia Damu ni Kuokoa maisha ya Mtu mmoja au zaidi,na hii ni Zawadi kubwa ambayo binadamu anaweza kuumpa binadamu mwenzie.
Imeelezwa kuwa kuchangia Damu mwanamke anaweza kuchangia mara tatu(03) kwa Mwaka na mwanaume anaweza kuchangia mara nne(04) kwa Mwaka.
Kwa kawaida mwili wa mwanadamu una damu galoni tano(05) hadi saba(07), na kwa kawaida unapochangia Damu kiasi cha Mililita 450 kinachotolewa.Mchangiaji hubaki na kiasi cha kutosha cha Damu hakuna haja ya kuwa na hofu.
MUHIMU:
Mtu yeyote mwenya magonjwa ya kurith haruhusiwi kuchangia damu.
Jumatatu, 5 Septemba 2016
HISTORIA YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
HISTORIA YA
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA BARA
Huduma ya zimamoto Tanzania Bara zilianza wakati wa utawala
wa Kikoloni mara tu baada ya vita vya pili vya Dunia mwaka 1945, na kwa kipindi hicho kulikuwa nakikosi kimoja kilichojulikana
kwa jina la POLICE
FIRE BRIGADE kilichosimamiwa na jeshi la Polisi.
Mnamo mwaka 1950
kikosi hiki kiligawanywa katika makundi mawili Zimamoto chini ya Halimashauri
za Manispaa na usimamizi wake ukawa chini ya Manispaa na kundi la pili ilikuwa
Zimamoto chini ya viwanja vya Ndege
chini ya usimamizi ya Idara ya Kazi kwa maana hiyo ilihama kutoka katika
usimamizi wa Jeshi la Polisi.
Kwa kuwa miji ilikuwa inakuwa kwa kasi hivyo basi vikosi
vingine vikaanzishwa na kimoja wapo ni kikosi cha Zimamoto bandari ambacho
kilikuwa chini ya usimamizi wa bandari.Mnanmo mwaka 1982 Zimamoto chini ya viwanja vya ndege ilihama na kuwa chini ya
usimamizi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi,wakati huohuo vikosi vya zimamoto
vilivyo kuwa chini ya Manispaa na miji viliwekwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za mikoa na serikari za mitaa(TAMISEMI)
Lengo la zimamoto kuanzishwa ilikuwa ni kutoa huduma ya
uzimaji wa moto pindi moto unapotokea na kufanya maokozi kwa ufanisi
zaidi,lakini kutokana na kuwa katika usimamizi wa mamlaka tofauti ufanisi wa
utendaji kazi wake haukuwaridhisha
viongozi wa serikali na ndipo serikali ikaamua kufanya mikakati ya kuboresha
huduma hiyo.
Katika bunge la Jamuhuri la Muungano wa Tanzania la mwaka 1985 sheria namba tatu(3) ilianzishwa
na kusababisa uanzishwaji wa Jeshi la Zaimamoto n Uokoaji lengo likiwa utowaji
wa huduma hiyo ya zimamoto itolewe katika taratibu na nidhamu ya kijeshi na kwa
kipindi hicho iliwekwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwakuwa lengo la uboreshaji wa huduma za zimamoto na uokoaji
zilikuwa bado zinahitajika,mnamo mwaka 2007
kwa mara nyingine tena Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha
sheria Na.14 ya Zimamoto na Uokoaji (Fire And Rescue Force Act) na baada ya hii
sheria jeshi la zimamoto na uokoaji liliwekwa chini ya Kamandi moja tofauti na
hapo awali.Kwa sheria hii Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilibadirisha muundo wa
Jeshi na kuweka mgawanyo mwa majukumu ilikuleta tija ili kurahisisha suala zima
la utowaji wa huduma za zimamoto na uokoaji.
Hivyo kwa sasa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaongozwa na
Kamishna Jenerali akisaidiwa na Naibu Kamishna Jenerali akifuatiwa na Kamishna
watatu wa divisheni tatu wanazoziongoza ambazo ni Utawala na Fedha,oparesheni
na Usalama wa umma na mali zao.
Katika divisheni hizi tatu kuna makamishna
wasaidizi wanaoziongoza ilikutengeneza mfumo wa utendaji wenye kuleta Tija na
katika utoaji wa huduma kwa jamii.
Kwa upande wa Usalama wa Umma idara
hii huusika na Kuzuia na kukabiliana na majanga ya aina yote kama
,Moto,matetemeko, Mafuliko na majanga mengine yanapotokea pia kufanya uchunguzi
wa vyanzo vya majanga yaliyokwisha tokea ili kupanga mikakati ya njisi ya
kukabiliana nayo.Pia huusika na utoaji wa elimu kwa umma juu ya majanga ya
moto,ukaguzi wa kinga na tahadhari ya majanga ya moto,Kukagua usalama wa ujenzi
katika viwanda vituo vya mafuta,kemikali na vituo vinavyo zalisha gesi na
kuhifadhi gesi.
Kwa upande wa Oparesheni miongoni
mwa majukumu yake ni pamoja na kusimamia mafunzo,kukagua huduma za zimamoto na
uokoaji kwa kanda na kufanya tathimini ya madhara yaliyotokea kwenye majanga
mbalimbali
Upande wa Utawala rasilimali watu na
Fedha majukumu yake ni kufanya utafiti na mafunzo,kusimamia uajili,kuandaa na
kutunza kumbukumbu za watumishi pamoja na maandalizi ya mpito ya sheria ya Moto
na uokoaji na kanuni zake.
Mbali na kuwa na changamotonyingi
lakini jeshi hili limekuwa na mafanikio makubwa moja wapo ikiwa ni kuanzishwa
kwa vituo vingi vya zimamoto takribani katika kila Mkoa na baadhi ya Wilaya
nchini,pia fanikio jingine ni suala zima la ushirikiano wa Jeshi la Zimamoto na
uokaji na majeshi Mengine kama vile
Magereza kwa kukubali mafunzo ya uaskari
kufanyika katika vyuo vyao kwa ngazi ya awali,uongozi mdogo,wakati na wajuu
kabisa.
Polisi kwa kukubali kutumia siraha
zao pindi zinapokuwa zinahitajika kwa mfano katika shughuli mbalimbali za jeshi
la zimamoto na ushirikiano mwingine wa majukumu ya kiulinzi katika nchi yetu
kwa ujumla.
Jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) kukubali baadhi ya askari wa
zimamoto kupatamafunzo katika chuo chao cha AirWing,Kimbiji vilivyopo Dar es
salaam,pamoja na kushirikiana katika majanga mbalimbali yenye kutishia maisha
ya watu na mali zao mfano,Mafuliko,Mlipuko wa mabomu ajari mbalimbali nk.
Pia kwa sasa Jeshi la zimamoto na
uokoaji Tanzania lina chuo chake binafsi kinachotoa mafunzo ya uaskari kwa
ngazi zote kuanzia mafunzo ya awali,vyeo vya kati na vya juu kilichopo wilaya
ya Handeni mokoaniTanga katika eneo liitwalo Chogo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
fc oscar mswima
Kumbukumbu la Blogu
-
▼
2016
(9)
-
▼
Septemba
(9)
- FIRE AND RESCUE FORCE MBEYA: Timu ya jeshi zimamot...
- Timu ya jeshi zimamoto mkoa wa mbeya yashiriki mic...
- Askari wa kikosi cha jeshi la zimamoto na uoko...
- UCHANGIAJI WA DAMU KUOKOA MAISHA Jeshi la Zi...
- Jeshi la zimamoto Mkoa wa mbeya latoa rai kwa wana...
- Askari wa jeshi la zimamoto mbeya wakiwa katika...
- HISTORIA YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
-
▼
Septemba
(9)